URIDU Afya Familia Kazi

Umuhimu wangu ni wa chini kuliko wa mvulana?

Njia ambayo mwanamke hujiona hubadilika akiendelea kukua. Ni muhimu kwa msichana kujifunza kujihisi vizuri akiwa kijana, ndio aweze kujiendeleza kabisa na kusaidia jamii yake iwe mahali pazuri. Msichana anaweza kujifunza haya ikiwa familia na jamii yake watamuonyesha kuwa, wanamthamini.

Mahali kwingi wasichana wanakuzwa kuamini kuwa umuhimu wao ni wa chini kuliko ya wavulana. Wanafunzwa kuona haya, aibu ya miili yao, kuwa wanawake, kukubali elimu kiasi, chakula kidogo, matumizi mabaya na kazi nyingi kuliko ya kaka zao. Hii haiumizi afya yao peke yake bali inawafanya wajihurumie na kukosa kufanya uamuzi sawa kuhusu maisha mazuri katika siku za usoni. Wasichana wakilelewa hivi, inaonyesha kuwa, jamii yao haiwathamini kama vile wanawathamini wavulana.

Lakini jamii ya msichana ikitambua thamana ya kila mtu - kama ni mume au mke - atakua akisikia kuwa yeye, familia yake na jirani zake wanaweza kuishi maisha mazuri.

Vile jamii inavyowachukulia wanawake huathiri vile familia zinachukulia watoto wao wasichana. Kwa mfano, kama jamii inaamini kuwa wasichana wanafaa kuwa na ujuzi, familia inayoishi hapo itataka pia binti yao aende shule kwa muda ule unaowezekana. Lakini kama ni jamii ambayo wanawake wanakubaliwa kufanya 'kazi ya wanawake' pekee yake na hawakubaliwi kujihusisha kwa mikutano ya umma, basi familia hazitaamini kuwa binti zao wanafaa kuelimishwa.