URIDU Afya Familia Kazi

Dalili/Ishara zipi za kutaka kujiua?

Kumbuka ya kwamba watu wengine wanaojiua huwa hawaonyeshi dalili zozote za kutaka kujiua kabla ya kujiua. Tena, wengi wao ambao hufa kwa kujiua huonyesha dalili zingine. Kwa hivyo ikiwa wamjua yeyote ambaye anaonyesha dalili zifuatazo za kujiua, fahamu ya kwamba anahitaji usaidizi wa dharura.
MUHIMU; Kuwa makini na ishara za kujiua. Ni ombi la usaidizi ambalo, kwa bahati mbaya halisikizwi. Wakati mtu anapokuambia ya kwamba anafikiria kujiua, kuwa makini na maneno hayo.