URIDU Afya Familia Kazi

Kwa nini wasichana wadogo hutamani kujiua?

Wasichana wanaofikisha umri wa kubalehe hupata changamoto na shida, haswa katika nchi zinazoendelea.
Wasichana wengi na wanawake vijana hukosa raha, huku wakikabiliana na shinikizo kutoka kwa (wanarika, familia, mtandao wa kijamii au sinema)wanaotarajia wakae na kuwa na vitendo aina fulani (kulingana na dhana ya urembo ulio bora). Wao huhisi hawavutii na hawastahili kupendwa na kukubaliwa. Hisia hizi zinaweza kuwafanya wajidhuru kama kujikata au kujihusisha na madawa ya kulevya.