URIDU Afya Familia Kazi

Kwanini kujiua ni tatizo kubwa kwa wanawake?

Kwa ujumla, vifo vitokanavyo na kujiua huwa mara tatu zaidi kwa wanaume ikilinganishwa na kwa wanawake. Hii yamaanisha: kwa kila kifo cha kujiua kwa wanawake, kuna vifo kama hivyo 3-4 kwa wanaume. Hata hivyo, katika kisa cha jaribio la kujiua ni kinyume yake: wanawake hujaribu kujiua mara tatu zaidi kila mara ikilinganishwa na wanaume.

Katika nchi zinazoendelea takwimu hizi hutofautiana kwa kiasi kikubwa. Idadi ya wanawake wanaojiua inazidi kuongezeka, na pengo kati ya idadi ya wanaume na wanawake wanaofanikiwa kujiua inazidi kupungua.

Wanawake vijana walioolewa katika nchi hizi wako katika hatari kubwa ya kujiua. Kwa mfano, katika eneo la kusini mwa India, idadi ya kujiua kati ya wanawake vijana ni ya hali ya juu ulimwenguni. Imegunduliwa ya kwamba, katika swala la vifo vinavyowahusisha wasichana kati ya miaka 15 na 19, wengi wao hufariki kutokana na kujidhuru wenyewe kuliko kutokana na ajali za barabarani, magonjwa(kama virusi vya ukimwi, ukimwi au homa) au shida zitokanazo na ujauzito.