URIDU Afya Familia Kazi

Je, ninapaswa kufahamu nini kuhusiana na kujiua?

Kitendo cha kujitoa uhai kwa kukusudia sababu ya kutotaka kuishi kinaitwa kujiua. Imekadiriwa kwamba vifo vya takriban watu milioni moja ulimwenguni kila mwaka huhusishwa na kujiua.

Hii inamaanisha kwamba kwa kila sekunde 40 ulimwenguni, mtu hujiua. Kadhalika, kuna visa milioni 20 vya kujiua kila mwaka vinavyotibuka na idadi hiyo inaongezeka.

Ni vigumu kupata idadi kamili ya visa hivyo kwani familia nyingi huficha maana kamili ya vifo vinavyosabishwa na kujiua, kwa kuhofia kudhulumiwa na polisi na wanainchi.

Huku visa vya kujiua vinapopungua kwa nchi zilizoendelea, visa hivyo vinaongezeka kwa idadi ya kushangaza kwa nchi zinazoendelea kustawi.

Sababu zinazoaminika kusababisha kujiua ni: